Thursday, 26 July 2007

Je unatumia au umewahi kutumia?


Madawa ya kuzuia mimba! Nimeombwa kutoa maelezo kuhusu hili jambo na mimi sina uzoefu nalo, hivyo tafadhali naomba ushirikiano wako mahali hapa.


Toa ushuhuda kuhusiana na swala zima la madawa hayo na mabadiliko, mafanikio n.k.


Kubaki na jambo bila kuchangia na wenzio ni uchoyo sio, haya karibu sana.


N:B Pamoja na maelezo yatakayo tolewa hapa wewe mwanamke hakikisha unamuona Dakitari kwa ushauri wa kitibabu kabla hujajikitakwenye hii kitu.


Nimebanwa kiaina na shughuli wiki hii.....unakumbuka nilizungumzia mikao ya kimazoezi, mikao inayosaidia ufike haraka sasa nikirudi naibuka na mikao ya kimahaba ambayo ni bab-kubwa sultani ka kipepeo ndani ya Dinahicious

10 comments:

Anonymous said...

Dina, hebu nieleze tafadhali... hiyo Ty mwisho unapotuaga ina maana/kirefu gani? si ushamba jamani... aulizae ataka kujua!

Dinah said...

Ni thanks=thank you ya kitoto (watoto wadogo huwa hawawezi kusema thank you na badala yake huesma "ta" ambayo ndio ty).

Anonymous said...

Asante dinah kwa kunielimisha kuhusu Ty.

shamim a.k.a Zeze said...

mi nasubiri huo mkao wa sultani...umenikumbusha mbaliiii!! enzi za ujana wangu

Mama Q said...

Sasa Shamim ulituahidi kutuletea mambo ya kukata kiuno umeyanasa huko kitchen party mbona hutuletei?au tukufuate huko 8020?lakni nadhani hapa ndo mahal pake kwa wanawake.

Anonymous said...

Mimi natumia birth control inayoitwa Yazmin. Its the best. Na miaka 30 na sikotayari kupata watoto - nilianza na Tri-Cyclen (the generic kind) lakini nikagain weight. Sasa nimeanza na Yazmin this May na nimelost weight. Naipenda sana maana periods get shorter and skin gets lighter and smoother. Nilicheki na daktari wangu na tulikumbaliana kuwa its the perfect prescription. Nitashauri kinadada wenzengu that Yazmin may be the right pill for you.

Eng. Alice said...

Tueleze mpenzi ni
Yazmin ipi maan naona ktk internet inaongelewa yazmin with drsp?? Which is better?? Na hapa bongo labda tutafute lkn sijawahi kuona, mwenyewe ambaye kaona tafadhali atujulishe wadau wengine tuweze kuvutiwa na kutumia!! Yaani hii blog naipenda sana inatusaidia kupata burudani na pia kuelimishana!! Inaonyesha watu wanaoipitia wengi wao ni wastaarabu!!
I like that ladies !! keep it up!!

Anonymous said...

Mimi natumia Yasmin with drsp (drospirenone). Yasmin with drsp is the best lakini cheki na daktari wako kabla ya kutumia. Mnaweza kuelimishwa zaidi kwenye website yao; http://www.yasmin.com
Sidhani kama Yasmin inapatikana bongo unaweza ukajaribu lakini mimi naipata kutoka New York (nafanya kazi huku).

Anonymous said...

okay asante !!kwa ushauri wako!! nitafatilia kujua hilo!! asante pia kwa website info!!
asante dinah pia!!

Mama Q said...

Dinah mpenz,pole na mihangaiko ya kila siku,Samahani kuna sehemu nilisoma umeelezea kuhusu vipele vinavotokea nyuma ya mapaja na pembeni,sasa sijakupata vzr embu nifahamishe mpenz mana ni tatizo langu,unatumia nin ili kuviondoa?