Saturday, 2 June 2007

Utatambua vipi kama ni yeye au sio?

UHUSIANO wa kimapenzi unaimarishwa na mambo mengi kutegemeana na wahusika wenyewe lakini haya matano (5) ambayo ni kusikilizana, kuaminiana, kuheshimiana, kusaidiana, kushirikiana ni muhimu na yakifuatwa vyema na pande zote mbili basi uhusiano wenu utakuwa mzuri na wenye afya.

Mara zote tunapoanzisha uhusiano huwa hatuko wazi kwa asilimia mia moja kusema tunataka nini kutoka katika uhusiano huo mpya. Mara zote sisi wanawke ndio huwa tunakuwa na kimbelembele kujua uhusiano tulionao unakwenda wapi katika kipindi kifupi, kwamba tunataka kufahamu kama ni “ring au fling” lakini kwa vile wanaume tunaokuwa nao kwenye uhusiano huwa hawataki kutukatisha tamaa au hanawana uhakika na hisia zao juu yetu wanawake hulazimika kutudanganya na baadhi hulipa na mahali kwa wazazi ili kutupa matumaini na at the end huwa hakuna ndoa.

Kwa wanawake inakuwa ngumu (baadhi hatujakuzwa hivyo) kuwaeleza wanaume kuwa tunachotaka ni uhusiano usio makini (casual) ili kukidhi mahitaji ya kifedha au kimwili na matokeo yake huwa tunatafuta njia za mkato ili kuwaudhi wenza wetu hali itakayo wafanya wamalize uhusiano na sisi.

Wanaume hujikakamua na kusema wazi ikiwa hawako tayari kuwa nauhusiano wa muda mrefu au hawako tayari kufunga ndoa kwa wakati huo na hivyo huturahisishia wanawake(ambao sio ving’ang’anizi) kuelewa uhusiano wenu utakwenda ama unakwenda wapi?.

Natambua kuwa kuna baadhi yetu huwa na uhakika kuwa uhusiano wao ni “ndoa” baada ya miezi mitatu ya kuwa pamoja na wengine huwachukua hadi miaka mitano kuwa tayari ama kuwa na uhakika na wanachokitaka kutoka kwenye uhusiano, hii ni kutokana na jinsi walivyokuzwa ama kushuhudia maisha mazuri au mabaya ya ndoa za wazazi wao au ndugu wakaribu.

Swala muhumi ni kuchukulia mambo taratibu na kutolazimisha (hasa kwa wanawake), ikiwa Mungu anataka kuwa huyo uliye nae ndio awe mume/mke wako basi ndivyo itakavyokuwa hivyo hali kadhalika ikiwa sio yeye hamtofika mbali hata kama utalazimisha atafunga ndoa na wewe kukuridhisha tu au kuhofia umri au hata kuhofia kudhaniwa Shoga na jamii inayomzunguuka.

Lakini ikumbukwe kuwa sote wake kwa waume hatuna mioyo ya ujasili wa kufanya hivyo na baadhi yetu huwa tunaonyesha kwa vitendo kuwa hatuko tayari kuuchukua uhusiano tulionao kwenywe hatua ya juu zaidi na badala yake huwa tunafanya vitendo bila kujitambua lakini vinaashiria wazi kabisa kuwa mtazamo wako na wa mwenza wako kwenye uhusiano wenu ni tofauti japo kuwa mnapendana kupita kiasi.

Vilevile kuna wakati unahisi ama unajua kabisa kutoka moyoni mwako kuwa humpendi sana mpenzi wako kama ambavyo ungependa kumpenda lakini unaendeleza uhusiano na yeye kwa kuhofia kumuumiza au kumuonea huruma ingawaje mwishoni mmoja kati yenu ni lazima atakumbana na ukweli na kuukubali ukweli huo kuwa hautakiwi.

Sasa, kuna vijimambo hujitokeza ndani yauhusiano ambavyo vitakufanya utatambue kuwa mpenzi wako hayuko makini sana na wewe au kakuchoka ila hajui jinsi yakutoka.

Uchelewaji: Mmeagana kukutana na wewe umesubiri kwa takriban saa nzima, lakini anapofika ana-act kuchelewa dakika tano tu na bila aibu wala huruma haombi msamaha kwa kukugandisha vilevile hatokupa sababu ya msingi/maana (mwanamke kuchelewa kwenye “date” ni muhimu na ni sehemu ya urembo ukiachilia mbali kujiandaa kuku-impress wewe bali pia umuone wakati anaingia na kukufanya wewe ujivunie kuwa na mrembo kama yeye).

Utani:Ni kitu kizuri na husaidia kuwaweka karibu kimapenzi, lakini ikiwa mwenza wakoa nakutania kuhusu mambo ambayo mnayafanya mkiwa wawili tu, au kasoro zako mbele ya rafiki zake, ndugu zake nakukucheka huo hautakuwa utani bali kukudhalilisha.

Kutotilia maanani: Mfano kuna swala muhimu unataka mzungumze lakini yeye anapiga tarehe kila unapoomba muda na yeye na siku akikubali kukaa chini ili mzungumze basi majibu yake yatakuwa ndio au hapana, hatoi maelezo ya kutosha kuhusiana na issue unayomueleza hasa ikiwa inahitaji maamuzi yenu kama wenza.

Kutojali: Wakati wote wewe ni mtu wa kupiga simu kujua yuko wapi, ikiwa anaumwa au anamatatizo kifedha wewe unakuwa pale kwa ajili yake lakini kibao kikikugeukia humuoni na wala haonyeshi kujali kuwa unamatatizo na kwamba anapaswa kuwa hapo kukupa moyo wa kukabiliana na yanayokukabili.

Sehemu ya mwisho ktk maisha yake: Kukatisha miadi na wewe kwa ajili ya kuonana na rafiki zake, wakati wote wote wewe ni mkosaji mbele ya wazazi wake na ndugu zake.

Kutengwa: Akitoka hatoki na wewe kwenda matembezini, kila akichelewa kurudi basi alikuwa na rafiki ambae hupaswi kumjua, hukutambulisha kwa jina lako badala ya “mpenzi wangu” ikifuatiwa na jina lako.

Kutoheshimu ndugu familia yako: Sote hatujakamilika, lakini ukikosea kidogo tu basi ukoo mzima utaunganishwa kwenye kosa hilo Mf ndio maana mama’ko yuko hivi, umerithi kutoka kwa baba yako, kwenu wote mko hivi au vile n.k.

Kwa leo naishia hapa tukutane tena baadae,

Upendo na amani ndio nguzo bora ya maisha marefu.

5 comments:

Anonymous said...

Nashukuru kwa maelezo yako yaliokwenda shule, naamini sio mimi tu niliyefaidika ni wengi tunafaidika.

Kaza kamba dada.

Much love!

shamim 'Zeze' said...

hallow bi shost kumbe umehamia huku mbona hunistui nije kupata mistariii....bora endelea kukamua kwa kujinafasii....NIMEKUSOMA

zeze!!

Dinah said...

Hahahaha karibu Zeze,Mbona nilikutumia link au iliingia kwenye bin? Yeah nimeamua kujinafasi ili wadada wanaonukiwa wapate mambo fulani kama wanapenda.

Dinah said...

Nafurahi sana kutambua kuwa umenufaika na kazi yangu, karibu sana. Hapa ni kwa ajili ya wanawake wote wa kibongo!

H. M said...

Dada Dinah, kwanza hongera kwa kazi nzuri ya kuelimisha akina mama, nimekuwa nikisumbuka kwa muda mrefu na nisipate jibu nimefurahi kuijua blog yako ninatumaini utanitatulia shida yangu, nina umri 28, nimeolewa mwaka jana na sijajaaliwa baby, nimekuwa nikilala na mume wangu kitanda kimoja wiki nzima bila kufanya chochote hali ya kuwa mimi ninakuwa na nyege na ninapojaribu kumpapasa amekuwa akigeukia upande wa pili na kuendelea kuvuta usingizi, atimae muda wa kuamka ukifika ninaamka na kujianda kwenda job,nimekuwa nikiumia sana kuhusu hilo swala na hawali hakuwa hivyo, sasa nashindwa kuelewa kamba anachoka sana ktk mihangaiko au amekuwa anamwanamke nje sipati jibu nisaidie dear, nipe mbinu nifanye nin, dinah na utundu wangu wote lakini pale nimekwama! nasubiri jibu kwako dada okoa jahazi nisije nikaingia tamaa nikatembea nje ya ndoa na atimae ndoa kuvunjika sitaki yatokee hayo plz tell me what to do.

kazi njema!